Friday, 10 October 2014

Hatimaye Jambazi Lililokuwa Likiwauwa Wanawake Jijini Arusha Lauwawa Baada ya Majibizano Makali ya Silaha na Polisi

           Tazama Picha Mbalimbali za Tukio Hilo
kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina laGlock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia...
 mwili wa Jambazi hilo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari


picha ya juu na chini  wananchi wa jiji la Arusha  waliojitokeza kuuangalia mwili wa  jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo





 wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha












 baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali



Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah  alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa  Moivo  ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari  wa jeshi la polisi.



Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10  mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku   katika  kijiji cha  Moivo  kilichopo ndani ya kitongoji cha  Enaboishu wilayani Arumeru.



Alisema kuwa marehemu  Ramadhan Abdallh  aliKuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya  mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.

Alibainisha  kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na  juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiupelelezi na kufika  nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru  ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia  mauti kumfika.



“Mara baada ya kumuua jambazi huyo polisi walianza kupekuwa  mwili wa marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi  na  mbali na hapo polisi pia  walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja  yeye nembo ya ITSS/UNICTR  pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU  pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas
 

Aidha alibainisha kuwa  pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD  ambapo alibainisha kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara  pamoja na  chombo maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi.

Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya  kuwa ni pamoja na tukio  lililotekea Augast 6  majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa  akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake, huku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo ya oasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na kutokea kichwani  mtoto aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.



Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.



“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu hivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote... na napenda kuwaambia wahalifu waache mapema maana sasa hivi tumejipanga vilivyo, pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu  popote pale ili tuwaangamize kabisa”alisema Sabas