Thursday, 9 October 2014

Je, unataka kuwa tajiri?...Basi Tazama ni Jinsi Gani Matajiri Wanatofautiana Kifikra na Masikini

Na Richard Thomas

Huu ni utafiti wa hivi karibuni...jaribu kutumia mda wako kuusoma ili kujiongezea kitu fulani katika maisha yako na katika fikra zako...


 
 Tabia  huifadhiwa kwenye ubongo katika sehemu inayoitwa basal gangliaHii ni sehemu yenye tishu nyingi iliyoko katikati ya ubongo na yenye ukubwa kama mpira wa golfuTabia huusaidia ubongo kazi....
Ubongo huusisha nguvu kidogo sana kulingana na tabia. Wakati tabia inapojijenga na kuhifadhiwa katika sehemu hii ya ubongo, sehemu nyingine za ubongo husimama kushiriki kikamilifu katika kutoa maamuzi kutokana na tabia hiyo.

Kitu cha kushangaza ni: 40% ya shughuli zetu za  kila siku ni tabia. Hii ina maanisha kwamba 40% ya muda tunaoutumia katika shughuli zetu huwa hatutumii ubongo kufikiri (on auto pilot). Huwa tunafikiri na kufanya mambo bila hata sehemu iliyobakia ya ubongo kuwa na ufahamu wa jambo lenyewe.Hatutambui ni kwa jinsi gani tabia ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Tabia hutufanya sisi kuwa kama tulivyo. 

Wazo lolote lililoko akilini, hususani lile linalojirudia mara kwa mara, hugeuka kuwa tabia. Mawazo uliyoyazoea ndiyo yanayokufanya wewe kuwa kama ulivyoWatu maskini ni maskini na matajiri ni matajiri kwa sababu ya jinsi walivyozoea kufikiri/  kutafsiri mambo mbalimbali. Mawazo waliyoyazoea huja kwanza na kisha shughuli walizozizoea kufuata. Kama umezoea kufikiri katika njia fulani utakuwa ukitenda katika njia hiyohiyo. Ufanisi unahitaji mawazo yenye ufanisi ndani yakeKuwa tajiri unahitaji kujifunza jinsi ya kufikiri kama mtu tajiri. Ili kuepuka umaskini hutakiwi kufikiri kama masikini.


Hebu tuangalie utafiti wa hivi karibuni kuhusiana na jinsi watu masikini wavyofikiri:



ï‚§ 87% ya watu maskini hufikiri lazima uwe na elimu ya hali ya juu ili kuwa tajiri
ï‚§ 90% ya watu maskini hufikiri kwamba kuwa na bahati huamua utajiri au umaskini wako katika maisha
ï‚§ 13% ya watu maskini hufikiri / hudhani watakuwa na mafanikio katika maisha
ï‚§ 11% ya maskini hufikiri ubunifu ni muhimu kwa mafanikio ya kifedha
ï‚§ 80% ya maskini hufikiri 
genetics (asili)  ni muhimu katika mafanikio
ï‚§ 18% ya maskini hudhani wao wenyewe ni sababu ya hali yao ya kifedha
ï‚§ 77% ya maskini hufikiri ili kuwa tajiri lazima uwe muongo
ï‚§ 2% ya masikini hukaa na kutafakari umasikini wao kila siku
ï‚§ 90% ya maskini hufikiri watu matajiri ni matajiri kwa sababu wazazi wao walikuwa matajiri na wao kurithi utajiri huo.
ï‚§ 22% ya watu maskini hufikiri matumaini chanya ni muhimu katika mafanikio
ï‚§ 5% ya watu maskini hufikiri watu matajiri ni wazuri, wanajituma na ni waaminifu
ï‚§ 52% ya watu maskini huamini utajiri ni kama ajalini bahati


Sasa Hebu Tuangalie Jinsi matajiri  wanavyofikiri Katika Mambo hayohayo:






ï‚§ 10% ya watu matajiri hufikiri lazima uwe na elimu ya hali juu ili kuwa tajiri

ï‚§ 10% ya watu matajiri hufikiri kwamba kuwa na bahati huamua hatima ya utajiri katika maisha yako.
ï‚§ 43% ya watu matajiri hufikiri / hudhani watakuwa na mafanikio katika maisha
ï‚§ 75% ya matajiri hufikiri ubunifu ni muhimu katika mafanikio ya kifedha
ï‚§ 6% ya matajiri hufikiri kuwa genetics (asili) ni muhimu katika mafanikio

ï‚§ 79% ya matajiri hudhani kuwa wao wenyewe ni sababu ya hali yao ya kifedha
ï‚§ 15% ya matajiri hufikiri ni lazima kuwa muongo ili uwe tajiri
ï‚§ 17% ya matajiri hukaa na kutafakari kila siku juu ya utajiri wao
ï‚§ 5% ya matajiri hufikiri kuwa watu ni matajiri kwa sababu wazazi wao walikuwa matajiri na wao kurithi utajiri huo
ï‚§ 54% ya watu matajiri hufikiri matumaini chanya ni muhimu katika mafanikio
ï‚§ 78% ya watu matajiri hufikiri kwamba watu matajiri ni wazuri, wanajituma na waaminifu
ï‚§ 4% ya watu matajiri huamini kwamba kuwa tajiri ni kama ajalini bahati tuu.


Kama unataka kuwa tajiri unahitaji kuacha kufikiri kama maskini na kuanza kufikiri kama tajiri; kuacha kutenda kama masikini na kutenda kama tajiri....GOODLUCK !


Utafiti wa:  Thomas C. Corley