KLABU ya Manchester United intake kucheza mechi za kirafiki za nguvu kuziba pengo la kukosa michuano ya Ulaya msimu huu na baada ya kutolewa katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup.
Mabingwa wa rekodi Ligi Kuu England, mara 20 pato lao limepungua kwa asilimia 10 msimu wa 2014-2015 baada ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha David Moyes.
Msoto huo umeifanya United ibaki na mechi moja tu ya katikati ya wiki kabla ya kumaliza mwaka 2014, na mechi tatu jumla katika miezi mitatu ya mwanzoni mwaka 2015.