Wednesday, 1 October 2014

Welbeck Ajeuka moto wa Kuotea Mbali: Apiga Hat Trick




Walisema ni fowadi mzigo? Leo watafunga midomo baada ya mshambuliaji Danny Welbeck kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.

Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi iliyopigwa ndani ya Emirates, bao jingine la Arsenal lilifungwa na Alexis Sanchez.

Welbeck aliyejiunga na Arsenal akitokea Man United, alipiga mabao mawili, Sanchez akaongeza la nne.
Galatasaray walipata bao la kwa mkwaju wa penalti baada ya kipa wa Arsenal kufanya faulo na kulambwa kadi nyekundu.

Pamoja na ushindi, Arsenal waliendelea kuonyesha kupania kufunga mabao zaidi ingawa walipotea nafasi kadhaa.