Thursday, 2 October 2014

Ebwana Kama una Tabia za Kuvaa Ngua za Jeshi au Zinazofanana na Jeshi Hii Inakuhusu..

Hii Imemtokea staa mwingine wa mziki wa Bongo Flavour.

nguo za jeshiKitu kama hiki kiliwahi kumtokea mwanahiphop Young Killer miezi michache iliyopita ambapo alivuliwa nguo ya jeshi aliyokua ameivaa…. wiki kadhaa baadae ikatangazwa tena kwenye vyombo vya habari kwamba ni marufuku kwa watu wasio Wanajeshi kuvaa nguo hizo....

Mwingine aliekutwa na mkasa huu ni msanii Linex akiwa Mbeya ambapo imefahamika  Wanajeshi walilazimika kuichukua suruali ya jeshi tukio lililomfanya ahojiwe na Soudy Brown wa clouds leo na kujibu >>> ‘nilikua nimevaa kama zinataka kufanana na nguo za jeshi, zinataka kufanana kwa mbali lakini sio nguo ya jeshi
Kwenye sentensi nyingine Linex akasema >>> ‘sikutaka kuwa mtata jamaa walikuja wakasema ile ni nguo yao nikaingia kwenye gari iliyokua imenipeleka Airport pale nikavua nikawapa sababu lazima niliheshimu jeshi la nchi yangu
LinexBig up kwa Wanajeshi waliofanya vile labda mimi ndio nilitakiwa kuwa mfano kwa watu wengine wanaozivaa mtaani, kwa ushauri tu ni kwamba Wanajeshi wapite kwenye maduka pia yanayouza nguo zinazofanana na nguo zao wachukue’ – Linex