Thursday, 2 October 2014

Maswali ya Msingi Ambayo Kila Mfanyakazi Anapaswa Kujiuliza

Maswali 8 ambayo kila mfanyakazi anapaswa kujiuliza
Maswali 8 ambayo kila mfanyakazi anapaswa kujiulizaBy Awali Mwaisanila on October 2, 2014@awaliambonisye
black-career-woman-400x295
black-career-woman-400x295
Tunapopata kazi mara nyingi tunasahau kufanya majumuisho ya namna ambavyo maisha yetu ya kazi yanaendelea......
Bali kuna maswali ambayo unatakiwa kujiuliza kuhusu maisha yako ya kazini ambayo ni pamoja na:

1. Je mimi ni mzuri kiasi gani katika kazi ninayoifanya?

Kama sina uhakika inabidi niulize kwa wenzangu, au kuangalia utendaji wangu kama unaendana na mategemeo yangu. Kama unahitaji kuboresha utendaji wako, omba msaada kwa wafanyakazi wenzako. Jaribu kufuatilia wale ambao wanafanya vizuri katika kazi zao na ujifunze kutoka kwao. Ongeza ujuzi wako kwa kusoma vitu mbalimbali vinavyohusiana na kazi yako, kupitia vitabu au njia ya mtandao ambayo ina vitabu vingi vya bure vitakavyoboresha utendaji wako kama utaweka juhudi katika kusoma.

2. Je nimekuwa si mwepesi kuomba msaada?

Mfano ulio wazi, napaswa kujiuliza ni mara ngapi naomba msaada? Je nimekuwa mtu ambaye narundikiwa kazi nyingi na wenzangu? Je nachukua kazi nyingi kuliko uwezo wangu? Je mimi ni mtu ninayepokea kuonewa bila kufanya chochote?

4. Je ninafanya kazi muda mwingi au masaa mengi zaidi?

Je kunakitu ninaweza kufanya au kuongea na bosi wako kama kuna uwezekano wa kupatiwa mtu mwingine ambaye mnaweza kugawana majukumu? Au kupunguziwa majukumu?

5. Je ninafanya kazi masaa machache ?

Kufanya kazi masaa machache hapa tunazungumzia kucheza michezo kwenye kompyuta, muda unaopoteza kwenye mitandao ya jamii, kuongea na watu na muda mrefu wa chakula cha mchana au lunch time. Je kuna mabadiliko yoyote ambayo nataka kufanya kuhusu hilo?

6. Je ninafanya kazi kidogo au nafanya kazi nyingi za kujitolea?

7. Je ninafikiria kubadilisha kazi?

Kama unafikiria kutafuta kazi nyingine, fanya utafiti kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kuacha kazi. Lakini kama una akiba ya kukutosha kukaa bila kazi kwa miezi mitatu hadi sita unaweza kufanya maamuzi ya kuacha kazi kama umeichoka.

8. Je nina bidii ya kupanda cheo au kushuka cheo?

Kupandishwa cheo sio njia pekee, wakati mwingine watu wengine wanafurahi zaidi wakiwa kwenye nyadhifa za chini kuliko kuwa juu.

Maswali hayo yanamaanisha nini?

Majibu yako yatakuonyesha wazi kitu gani ambacho unatakiwa kufanya. Inawezekana unaonekana kuchoshwa na kazi wakati majibu yako yanaonyesha hakuna tatizo, unachotakiwa kufanya ni kujibu kwa umakini na kuangalia ukweli wako katika maisha yako ya kazi. Kama hakuna kitu kinachokusumbua, hongera inawezekana umeridhika na kazi unayofanya.