kumekuwa na mgogoro mkubwa sana kati ya Wenger na Morinho ambao nadhani kwa upande mkubwa umekuwa ukichangiwa na vyombo vya habari...hii ni kutokana na kutoa taarifa ambazo ni za kejele kutoka kwa Morinho dhidi ya Wenger......chuki hii ilizidi kuwa kubwa pale Morinho alipotoa kauli yake kuwa Wener ni professional failure, na hivyo kukuza chuki dhidi ya makocha hawa wawili. Hata hivyo Morinho aliweza kuthibitisha haya baada ya kumfunga tena kwa mara nyingine na kusababisha Prof. Wenger kushindwa kuzuia hisia zake juu yao na kufikia hatua hata ya kumsukuma na kuzua mijadala mingi sana katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.





ifuatayo ni rekodi ya makocha wanaoziongoza timu hizo Jose Mourinho wa Chelsea dhidi ya Arsene Wenger wa Gunners.
Kwa mujibu wa rekodi zilizotolewa na BBC – Wenger na Mourinho wamekutana mara 11 katika mechi za Barclays Premier League.
Katika mechi hizo 11 – Mourinho ameiongoza timu ya Chelsea kushinda mara 6 na kutosa sare 5, huku Wenger akiwa hajawahi kuambulia ushindi dhidi ya mpinzani wake.
Wenger ameiongoza Arsenal kufunga jumla ya magoli sita dhidi ya Chelsea – wakati Mourinho ameiongoza Chelsea kufunga jumla ya magoli 19 dhidi ya Gunners.
